Tite atangazwa kama kocha mpya wa Brazilia
Rais wa klabu ya Corinthians Roberto de Andrade ametangaza kuwa Tite amekubali kumrithi Dunga kama kocha wa timu ya taifa ya Brazilia, akiacha wadhifa wake katika klabu, Goal imebaini.
“Profesa Tite hadi sasa si kocha wa Corinthians, na hatakuwa katika udhibiti wa mchezo wa Alhamisi,” Rais aliwaambia waandishi wa habari.
“Cleber Xavier, Matheus, mvulana wake, na Edu Gaspar pia wataondoka naye.”
Dunga na mratibu wa timu ya taifa Gilmar Rinaldi walifutwa kazi Jumanne baada ya utendaji hafifu wa Brazilia katika Copa América Centenario.
Meneja wa zamani wa Corinthians atakuwa kocha wa nne kufunza Selecao katika kipindi cha miaka minne iliyopita, baada Mano Menezes, Luiz Felipe Scolari na Dunga
No comments