TP Mazembe njia panda, Zamalek, Zesco wang’ara Ligi ya Mabingwa Afrika
Winga wa Yanga, Issoufou Boubacar akiwatoka walinzi wa Al Ahly ( Picha Soka360)
Bingwa mtetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya TP Mazembe imeangukia pua kwa Wydad Casablanca ya Morocco. Wenyeji Wydad wameicharaza TP Mazembe kwa mabao 2-0 katika pambano la hatua ya 16 Bora lililochezwa Jumamosi usiku.
Mabao ya Abdellatif Nousir na Reda El Hajhouj kupitia kwa mkwaju wa penati yalitosha kuwazamisha wawakilishi wa Kongo na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Nako nchini Mali wenyeji Stade Malien walishuka dimbani kuwakabili Zesco United. Katika mchezo huo wenyeji Stade Malien wamejiweka katika hali ngumu baada ya kucharazwa mabao 3-1.
Mabao ya Zesco United yalifungwa na Idris Ilunga Mbombo aliyefunga mawili na Mwape Mwelwa, huku bao pekee la Stade Malien likifungwa na Moussakoye Diallo.
Nchini Sudan, wenyeji Al Merrikh wamejiweka katika mazingira magumu baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na miamba ya soka la Algeria, ES Setif.
Mabao ya Al Merrikh yalifungwa na Raj Abdel Aati aliyeziona nyavu mara mbili huku Eudes Dagoulou na Abdoulmoumene Djabou wakiifungia ES Setif.
Nchini Misri, Zamalek waliitumia vizuri fursa ya uenyeji kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria. Mashujaa wa Zamalek walikuwa ni Mahmoud Kahraba na Ahmed Hamoud.
Matokeo yote ya Mechi za mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika
Young Africans (Tanzania) 1-1 Al Ahly ( Misri)
Wafungaji: [Ahmed Hegazy (Alijifunga)] [Amr Gamal]
Al Merreikh ( Sudan) 2-2 ES Setif ( Algeria )
Wafungaji: [Raji Abdel Aati 2x] [Eudes Dagoulou, Abdoulmoumene Djabou]
Wydad Athletic Club ( Morocco) 2-0 TP Mazembe ( JK Kongo )
Wafungaji: [Abdellatif Noussir, Reda El Hajhouj (pen.)]
ASEC Mimosas ( Ivory Coast) 2-0 Al Ahli Tripoli ( Libya)
Wafungaji : [Dao Youssouf, Aka Serge]
Zamalek ( Misri) 2-0 MO Bejaia ( Algeria )
Wafungaji: [Mahmoud Kahraba, Ahmed Hamoudi]
Stade Malien ( Mali ) 1-3 ZESCO United ( Zambia )
Wafungaki: [Moussakoye Diallo] [Mwape Mwelwa, Idris Ilunga Mbombo 2x
No comments