HAYA NDIYO MAAMUZI YA MGODI WA GEITA BAADA YA GEITA GOLD SPORTS KUJIHUSISHA NA UPANGAJI MATOKEO
Mgodi wa dhahabu wa Geita ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Geita Gold Sports umesitisha udhamini wake kwa muda kwa klabu hiyo inayotuhumiwa kupanga matokeo ya ligi daraja la kwanza.
Msemaji wa mgodi huo Tenga bin Tenga amesema licha ya Geita Gold Sports kuwaandikia barua ya kujitetea kwamba haihusiki na kashfa hiyo, mgodi kwa sasa hautahusika na udhamini wowote hadi pale ukweli halisi wa tuhuma hizo utakapobainika.
“Baada ya tu ya timu kutuhumiwa kwamba imetumia rushwa na kupanga matokeo, haraka uongozi wa mgodi wa Geita ukaiandikia timu barua kwamba iwezekutoa ufafanuzi wa jambo hili ambalo linazunguzwa”, amesema Tenga.
“Timu ilichofanya, ilijibu na kusema hawana hatia yoyote na hawajafanya kitendo kama hicho lakini kama uongozi unahakikisha sheria na taratibu zinafuatwa, mgodi ulichofanya ni kusitisha udhamini tukisubiri upelelezi na uchunguzi wa TFF pamoja na chunguzi nyingine ili ziweze kutoa majibu yanayofaa katika kufanya maamuzi”.
“ Kwahiyo kwasasa mgodi umesitisha udhamini ukitegemea kutoa maamuzi sahihi pale ambabo taratibu zote za uchunguzi zimeshapata majibu”.
Msemaji huyo pia akazungumzia namna mgodi huo ulivyopokea taarifa za hukumu ya shirikisho la soka nchini (TFF) hivi karibuni.
“Kuhusiana na hukumu iliyotolewa na TFF ilitushtua sana kwasababu jamii na watu wote ambao ni wadau tunaojishughulisha nao tunaamini kwamba watafanya vitu sawasawa na mgodi vile ambavyo unafanya. Mgodi unatii taratibu na sheria za nchi, mambo ya rushwa na upangaji wa matokeo ni vitu ambavyo mgodi unapinga sana”.
“Kwahiyo TFF kusema kwamba timu ya Geita imejihusisha na rushwa imetushtua na imetusikitisha kwahiyo uongozi utakaa na utatuambia tunafanya nini”.
No comments