GONZALO HIGUAIN HAKAMATIKI SERIE A
Juzi Jumapili, mshambuliaji wa Napoli na timu ya taifa ya Argentina Gonzalo Higuain aliifungia timu yake ya Napoli magoli mawili katika ushindi wa bao 3-1 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya 6 Sassuolo katika muendelezo wa ligi kuu nchini Italia, Serie A.
Magoli hayo mawili ya Higuain ambaye amekua katika msimu mzuri sana tangu kuanza msimu huu, yamemfikisha hadi goli la 20 weekend iliyopita na kukaa juu kabisa ya ufungaji wa magoli huku Napoli wakiketi kileleni mwa msimamo huo kwa tofauti ya points nne.
Katika mchezo wao dhidi ya Sassuolo Jumapili iliyopita, Sassuolo ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao, Diego akifunga katika dakika ya tatu tu ya mchezo kwa njia ya penati kabla ya Jose Maria Callejon kusawazisha katika dakika ya 19.
Gonzalo Higuain akionesha makucha yake, aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 42 kabla ya kuhakikisha ushindi dakika za nyongeza mpira ukiwa unaelekea kuisha.
Napoli hawajapoteza katika michezo 19 mfululizo tangu walipofungwa na Sassuolo siku ya ufunguzi wa ligi mwanzoni mwa msimu na sasa wamejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa nchi hiyo ‘scudeto’.
Inaelezwa kua fomu hii ya Gonzalo Higuain inachagwizwa na mfumo wa kocha mpya aliyerithi mikoba ya mhispania Rafael Benitez ambaye alikua akimsimamisha Higuain peke yake mbele, kabla ya kocha mpya kupanga washambulizi watatu mbele na kumpa fursa Higuain kuwa na usaidizi mkubwa langoni mwa wapinzani
No comments