BAADA YA KUTUNDIKA DARUGA, HII NDIYO MECHI YA KUKUMBUKWA NA CANNAVARO MAISHA YAKE YOTE AKIWA STARS
Baada ya kupeleka barua kwenye shirikisho la soka Tanzannia (TFF) kutangaza kustaafu soka la kimataifa, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameitaja mechi ambayo hatoisahau kwenye maisha yake tangu alipoanza kuitumikia Stars.
Cannavaro amesema mechi ambayo bado ipo kwenye kumbukumbu zake siku zote ni ambayo Stars ilikubali kufungwa goli na Zambia dakika za lala salama ikiwa imesalia dakika moja tu mwamuzi amalize mchezo huo lakini Zambia walikwamisha mpira wavuni na kuitupa Stars nje ya mashindano. Mechi hiyo ilikuwa ya michuano ya kwanza ya CHAN iliyofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
“Mechi ya timu ya taifa ambayo siwezi kuisahau ni ile ambayo tulifungwa na Zambia katika mashindano ya CHAN, kama tungeweza kustahimili kwa dakika moja basi tugeweza kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Inaniuma hadi leo, tukarudi nyumbani tukiwa vichwa chini”, amesema Cannavaro.
Shadrack Nsajigwa aliyekuwa nahodha wakati huo aliifungia Tanzania bao dakika ya 88 kwa mkwaju wa penati lakini Zambia walizima matumaini ya Tanzania kusonga mbele kwa kusawazisha goli hilo kupitia Banda dakika ya 90+4 na kuiondosha Stars kwenye mashindano.
Tanzania ilimaliza ikiwa ya tatu kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne nyuma ya Zambia na Senegal ambazo zote zilikuwa na pointi tano na zikafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali. Tanzania ingefanikiwa kumaliza kwa ushindi kwenye mechi hiyo ingeongoza kundi A baada ya kufanikiwa kuifunga timu mwenyeji Ivory Coast kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Ngassa.
Cannavaro ametangaza kustaafu soka la kimataifa akilalamikia utaratibu uliotumika kumvua kitambaa cha unaodha na kumpa Mbwana Samatta ambapo nahodha huyo mkongwe anadai hakupewa taarifa rasmi badala yake alipata taarifa kupitia vyombo vya habari. Cannavaro anadai hakupewa heshima kama mcheaji ambaye amelitumikia taifa kwa zaidi ya miaka
No comments