SAMATTA AWA GUMZO MITAA YA ALGERIA
Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria
Kikosi cha wachezaji 21 cha wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, benchi la ufundi pamoja na viongozi wengine wa TFF tayari wapo nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kucheza fainali za michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Kitu cha kuvutia katika mitaa mbalimbali nchini Algeria ni jinsi ambavyo jina la Mbwana Samatta lilivyokaa midomoni mwa waalgeria wengi kitu ambacho kimepelekea kila raia mweusi anayeonekena ana-asili ya Tanzania amekua akiitwa Samatta.
Iyo ni kutokana na uwezo mkubwa ambao umeoneshwa na mchezaji huyo katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya timu ya USM Alger ya Algeria ambapo Samatta alifunga magoli mawili katika mechi zote mbili walizocheza.
Watanzania wanaosoma nchini Algeria wamethibitisha kuwa, Samatta amekuwa gumzo kubwa kwenye mitaa mbalimbali ya miji ya Algeria.
“Mtaani huku story kubwa ni Samatta, ukipita umevaa jezi ya Tanzania unaitwa Samatta. Sasa inabidi jamaa alilinde jina lake afanye kweli lkazi na wachezaji wengine akina Thomas Ulimwengu, Ngassa na wachezaji wengine wafanye kazi”, amesema mwanaunzi mmoja mtanzania anayesoma Algeria lipozungumza na Yahya Mohamed.
Samatta alifunga goli moja kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Algeria kwenye sare ya magoli 2-2 na kufanya nyota huyo kufunga magoli matatu dhidi ya timu za Algeria ndani ya mwezi mmoja.
Stars leo itafanya mazoezi saa 1:00 usiku kwa saa za Algeria sawa na saa 3:00 kwa saa za Afrika Mashariki kabla ya kesho kuingia uwanjani kupambana na ‘Mbweha wa Jangwani’
No comments