Recent Posts

Washindi Ligi ya Uingereza hadi sasa: United walamba Dume huku Ranieri akionesha yeye ni fundi

 Washindi Ligi ya Uingereza hadi sasa: United walamba Dume huku Ranieri akionesha yeye ni fundi
MYSPORTBASE inakuletea uchambuzi wa washindi na wachemkaji wa Ligi ya Uingereza mapema msimu huu. Tukianza na washindi
Mourinho amekuwa akiwadhihaki Claudio Ranieri, Arsene Wenger na Manuel Pellegrini. Sasa wote wapo katika nafasi sita za juu msimamo wa Ligi Kuu.
Mechi nane, Chelsea wametoka kwenye hali mbaya kwenda kwenye hali mbaya zaidi. Klabu zote zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kila moja imepoteza angalau mechi mbili. Matokeo ya mechi nyingi yamekuwa ya kushangaza. Ushindi wa mechi za ugenini umezidi ule wa nyumbani. Wayne Rooney na Diego Costa wameshindwa kupata magoli.
Pamoja na ugumu wa Ligi ya Uingereza msimu huu, mysportbase inakuletea uchambuzi wa washindi na wachemkaji wa Ligi ya Uingereza mapema msimu huu. Tukianza na washindi
WASHINDI
Anthony Martial
Ni nani? Thamani yake? Ujio wa Martial katika Manchester United ulizua mijadala. Wangetumia paundi milioni 58.8 kumsajili kipanga huyo. Dakika 21 za mwanzo katika mechi yake ya kwanza na, kwa kasi, umahiri na utulivu kama wa Thierry Heny alifunga dhidi ya Liverpool.


Slaven Bilic
Lilikuwa zali la kihistoria. Hakuna yeyote aliyewahi kushinda katika viwanja vya Emirates, Etihad pamoja na Anfield ndani ya msimu mmoja.
Bilic alifanya hivi katika mechi zake tatu za kwanza za ugenini kama meneja wa West Ham.


Claudio Ranieri
Hakuna aliyedhani kuwa Muitaliano huyo angepewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Nigel Pearson. Lakini ameiendeleza vema klabu ya Leicester kutoka pale alipoiacha mwenzake.
City wameshambulia na kushinda. Kwa kiasi fulani Ranieri amemfanya Jamie Vardy kuwa kinara wa mabao Ligi ya Uingereza.
Crystal Palace
Inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi ya Uingereza ikiwa na pointi 15 nyuma ya Manchester United na Arsenal zenye pointi 16.
Walipata ushindi dhidi ya Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge
Yohan Cabaye ameleta chachu katika kikosi hicho wanapokuwa dimbani na timu hiyo ya Alan Pardew wamekuwa wafalme wa barabara kwa rekodi nzuri ya mechi za ugenini.

Kevin De Bruyne
Ada kubwa za usajili zilipaswa kuwa mzigo kwa wachezaji. Si kwa De Bruyne!
Mbelgiji huyo aliyeigharimu Manchester City paundi milioni 54 amepata fursa ya kuanza mechi tano tu tangu alipotua Etihad akitokea Wolfsburg lakini tayari ameshafunga magoli manne na kutengeneza mengine matatu.

Washindi wengine
JAMIE VARDY: Alifunga magoli matano Ligi Kuu msimu uliopita. Msimu huu ana magoli saba tayari.
ANDRE AYEW: Mchezaji aliyetua Swansea kwa uhamisho wa bure amefunga goli dhidi ya Chelsea, Manchester United na Spurs.
VINCENT KOMPANY: City wameruhusu goli moja tu huyu bwana alipokuwa dimbani.

No comments