Wachezaji watano watukutu kwenye historia ligi ya Epl
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ametajwa kuwa mchezaji mwenye tabia chafu zaidi katika ligi kuu Uingereza msimu huu, baada ya kuondoka kwa Mario Baloteli na Joey Barton.
Lakini mbali na Costa hii ndio listi ya wachezaji wengine waliowahi kuwa na tabia kama hizo kuwahi kutokea katika historia ya EPL katika nyakati tofauti tofauti.
5. Scott Parker
Kiungo huyu wa Kiingereza amejikusanyia kadi takribani 86 za manjano katika muda wote aliocheza ligi kuu Uingereza akiwa na vilabu vya Chelsea, Newcastle United, West Ham United,Tottenham Hotspur na Fulham(kabla haijashuka daraja).
4. Patrick Vieira
Alisajiliwa na Arsenal akitokea kunako klabu ya Inter Milan, kiungo na nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, alikuwa ni mpinzani mkubwa wa nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane ambaye pia alisifika kwa tabia chafu.
Licha ya kubeba makombe matatu ya EPL likiwemo lile ambalo walimaliza ligi bila ya kufungwa , Vieira ndiye nahodha pekee wa Ligi Kuu Uingereza kupata kadi mbili za manjano katika matukio sita kwenye mchezo mmoja na kuonyeshwa kadi mbili nyekundu. Katika kipindi chote cha maisha yake ya soka Vieira alipenda sana migongano na wachezaji wenzake kama Roy Keane.
3. Kevin Davies
Huyu ni nahodha wa zamani wa Bolton Wanderers amefanya na kufanyiwa faulo nyingi zaidi katika historia ya Ligi Kuu nchini Uingereza.
Alicheza katika klabu kadhaa katika miaka yake 22 ya maisha yake ya soka zikiwemo Southampton, Bolton Blackburn Rovers.
2. Paul Scholes
Kiungo huyu wa zamani wa Manchester United ni mchezaji wa tatu kwa kuonyeshwa kadi za njano nyingi zaidi katika historia ya Ligi Kuu Uingereza nyuma ya mshambulizi wa zamani wa Bolton Kevin Davies na kiungo wa zamani wa Newcastle Lee Boywer.
1. Vinnie Jones
Huyu unaweza kumwita mchezaji mgumu kuliko kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka, Jones anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kupewa kadi kwa haraka zaidi katika mchezo rasmi, akipewa kadi baada ya sekunde tatu tu kwenye mchezo wa kuwania kombe la FA mwaka 1992 wakati akikipiga kunako klabu ya Chelsea.
Jones ametolewa nje katika matukio sita tofauti katika Ligi Kuu nchini Uingereza, akizawadiwa jumla ya kadi nyekundu 12 katika maisha yake yote ya soka na kufunga ukurasa wa wachezaji wenye nidha
No comments