Recent Posts

Straika aliyetemwa na simba aongoza kwa magoli VPL

Elius Maguri, Mshambuliaji wa Stand United anaetesa baada ya kutemwa Msimbazi

Mshambuliaji wa Stand United Elius Maguri anasimama kama kinara wa mabao kwa sasa kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa na mabao sita baada ya kupasia nyavu mara mbili kwenye ushindi wa goli goli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa juma lililopita.

Maguri amempiku mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza na Donald Ngoma wa Yanga ambao kila mmoja amefunga magoli matano wakifuatiwa na Amis Tambwe wa Yanga na Kipre Tchetche wa Azam wenye mabao manne kila mmoja.

Mshambuliaji huyo ambaye anang’ara kwa sasa akiwa Stand United ‘Chama la Wana’ alitemwa na klabu yake ya Simba iliyomsajili akitokea Ruvu Shooting kwa madai kuwa uwezo wake ni mdogo.

Maguri ndiye mfungaji mwenye magoli mengi pia kwenye timu ya Stand kwani anaemfutia ana goli moja tu kati ya magoli saba mbayo timu hiyo imeshafunga hadi sasa.

Mpaka sasa Maguri ameisaidia Stand kufikisha pointi 12 na kukaa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi saba na kufanikiwa kushinda mechi nne huku wakiwa wamepoteza mechi tatu.

No comments