Recent Posts

Star huyu wa real madrid kuhudhuria mahakamani siku ya mechi ya el clasico


Karim Benzema hataweza kucheza mechi ya El Clasico kwa sababu siku ya mechi hiyo ndio tarehe yake ya kuhudhiria mahakamani. [Caden Ser]

Hili ni jambo ambalo anakumbana nalo Karim Benzema wakati wa mechi ya El Clasico 21 Novemba ni tarehe ambayo inaingiliana na tarehe yake ya kuhudhuria mahakamani kutokana na kuvunja sheria za barabarani.

Kulingana na kituo cha redio cha Cadena Ser nchini Hispania, mshambuliaji huyo mfaransa anatakiwa kuhudhuria mahakamani tarehe 21 Novemba kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa na leseni mjini Madrid.

Inawezekana Benzema akaweza kufanya vyote kwa pamoja akaenda mahakamani asubuhi na jioni akaenda kucheza mechi hiyo japo itakuwa inavuruga maandalizi ya mechi hiyo kwa kocha wake Rafa Benitez.

No comments