Recent Posts

Ronaldo: Nitastaafu Madrid, nikifikisha miaka 36.

Cristian Ronaldo hana mpango wa kuondoka Real madrid na anaamini ana uwezo wa kucheza miaka 6 mingine zaidi kama akijichunga vizuri.

Kulikuwa na tetesi kuwa Ronaldo anaweza kurudi klabu yake ya man united au kuelekea klabu ya PSG kama angeondoka man united.

Hata hivyo mkataba wa Ronaldo Real madrid unatarajia kuisha 2018, anasisitiza kuwa anatamani kuendelea kubaki madrid na kustaafu maisha yake ya mpira akiwa ligi ya hispania.


Ronaldo:"Ndoto zangu ni kustaafu soka nikiwa Real madrid, kama mtu ukijichunga vizuri unaweza ukacheza mpaka ukafikia miaka 40."

"Nataka kuendelea kucheza mpira kwa miaka mitano mpaka sita ijayo. Na nimepanga kuendelea kufunga wastani wa magoli na mechi kama ilivyo sasa."

“I feel good and useful at Madrid, I want to keep winning here.”
"Najisikia vizuri na kutumika Madrid, nataka kuendelea kushinda nikiwa hapa." Amesema haya kupitia chombo cha habari cha Marca nchini hispania

Ronaldo alishinda kiatu cha dhajabu kwa mara ya nne na hakuna mchezaji mwingine aliyefikia hiyo idadi na ameonyesha kuwa anatamani kushinda kiatu hicho zaidi

No comments