Recent Posts

PIGO LA MANCHESTER CITY KWENYE MECHI VS MANCHESTER UNITED

October 25 Manchester City watakua na mechi muhimu dhidi ya Manchester united. Hadi sasa Manchester city imepata pigo kwa mchezaji wao muhimu Kun Aguero baada ya kupata jeraha akiwa anacheza na timu yake ya taifa.

Aguero alishidwa kuendelea na mechi na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Tevez. Kila mtu anajua Aguero ni mchezaji muhimu sana kwa Man city ambapo wiki iliyopita aliweza kufunga magoli 5 peke yake.

Ripoti zaidi kuhusu jeraha la Aguero inasemekana kwamba alitokwa machozi kwa maumivu makali akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kutolewa alivyotolewa uwanjani. Jeraha hilo inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi hiyo muhimu. Ikumbukwe pia Aguero alipata jeraha kwenye EPL wiki kadhaa zilizopita

No comments