ORODHA YA WACHEZAJI WANAOMCHUKIA WENGER KUPITA KIASI….
5. Emmanuel Frimpong
Hasira za Frimpong kwa Arsenal na Arsene Wenger zinaonekana kuongezeka kila siku. Mwaka 2014 majira ya joto, alimkosoa Wenger kwa kutumia fedha nyingi sana kumnunua Sanchez badala ya kununua kiungo mkabaji.
4. Dennis Bergkamp
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp ni nguli klabuni hapona ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Arsenal lakini ukweli ni kwamba hakuwa na mahausiano mazuri na kocha wake Arsene Wenger jambo ambalo litawashtua wengi juu ya hili.
“Wakati mwingine namchukia sana kocha wangu,” Bergkamp aliiambia News of the World.
“Inahuzunisha sana kutokucheza wakati uko vizuri bila ya shaka yoyote ile.
“Mbona ni rahisi tu, Wenger huamini sana katika kupumzisha wachezaji lakini mimi sipendi.
“Na nimeshamweleza hili mara nyingi kwamba sipendi suala hilo hasa pale ninapofanyiwa mabadiliko wakati huo huo nacheza vizuri.
Mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi alikuwa katika kikosi cha Arsenal cha mwaka 2003/04 kilichochukua ubingwa bila kufungwa.
3. Nicklas Bendtner
“Nilicheza mara kwa mara nilipokuwa Juventus mpaka nilipopata majeraha. Nikiwa hapa Arsenal nilicheza mara chache sana. Mwaka wangu wa mwisho ulikuwa ni kama umepotea tupu vile.
“Sisi ni mabingwa, nilitaka kusema. Lakini Arsenal imenirudisha nyuma. Nilipoteza mwaka mzima pale .Hilo limenichukiza sana.”
2. Emmanuel Adebayor
Mchezaji huyu ambaye ametupiwa virago na Tottenham Hotspurs hatomsahau mzee huyu. katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Manchester City, mchezaji huyo wa kimataifa wa Togo alifungiwa na FA kwa kushangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal. Ushangiliaji wake ulizusha mtafaruku uwanjani hapo.
“Mawazo yangu ni kwamba Emmanuel Adebayor anastahili kupewa adhabu kwa kile alichokifanya,” alisema Wenger.
“Lakini nilishangazwa sana na uadui wa namna ile na mtazamo wake juu ya Arsenal kwa sababu ndani ya miaka michache atakuja kutambua kwamba Arsenal imekuwa ni msaada mkubwa sana kwake”. “Nilishangazwa sana na kushtushwa. Nadhani kadiri muda utakavyokwenda atakuja kujua kwamba Arsenal ilikuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yake,” Wenger alisema.
1. Gervinho
Staa huyu wa AS Roma, Gervinho ambaye alicheza Arsenal kati ya mwaka 2011-2013 na kufunga magoli 9 katika mechi 46 alimkashifu bosi wake wa zamani Arsene Wenger kwa kile alichokiita kwamba hakumjali wakati akiwa klabuni hapo.
“Wenger kamwe hakuniamini. Kocha wa Roma Rudi Garcia huwa hatofautishi kati ya wachezaji ambao hupata nafasi ya kucheza na wale wasiopata fursa. Hilo ni suala muhimu sana kwa mchezaji”, alisema.
“Sio kana kwamba haongei na wale wanaocheza, bali anaongea na kila mtu kwa sababu kuna wachezaji 25 na sio tu 11.
“Kama mtoto, nilikuwa na ndoto kubwa sana za kucheza Arsenal kwa sababu niliipenda sana ile timu”.
“Lakini kwa sasa nawachukia kutokana na namna Wenger alivyonifanyia”.
“Hata hivyo, najutia sana maamuzi yangu ya kuondoka klabuni hapo mapema mno kwa sababu sikupata nafasi ya kuonesha makali yangu, kitu ambacho badala yake nakifanya hapa Roma instead ya Arsenal"
No comments