Recent Posts

Matokeo ya mechi zote za Uefa usiku wa Jumatano

Usiku wa October 21 michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea tena kwa michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Usiku wa October 21 ilipigwa michezo nane kutoka katika timu zilizomo katika Makundi A, B, C na D. Makundi ambayo yana timu zaReal Madrid na Paris Saint Germain.

Mchezo wa Kundi A uliyokuwa unazikutanisha timu za Paris Saint Germain ya Ufaransa dhidi ya Real Madrid ya Hispania ulikuwa ni mchezo ambao ulivuta hisia za watu wengi, mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Parc des Princes nchiniUfaransa, ulimalizika kwa timu zote mbili kutofungana na kuishia kwa sare ya 0-0.

Vilabu vya Real Madrid ya Hispania naParis Saint Germain ya Ufaransa vina wachezaji mastaa kama Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic hivyo wengi walitegemea kuona mastaa hao wakifunga magoli mengi ila mambo yamekuwa tofauti kwa nyota hao kushindwa kutamba kwa kupachika goli na mchezo kumalizika kwa sare ya kutofungana magoli.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwaOctober 21

No comments