Recent Posts

Majina ya wachezaji 23 wanaowania Ballon D'or 2015 haya hapa

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha ya wachezaji 23 ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora duniani kwa mwaka 2015 (the 2015 Ballon d’Or)

Mshindi mara nne wa tuzo hiyo Lionel Messi na anaeishikilia tuzo hiyo kwa sasa Cristiano Ronaldo, wote wapo kwenye orodha hiyo uku Gareth Bale akiwa ni moja kati ya wachezaji walioingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Bale ametajwa kwenye orodha hiyo kutokana na kiwango kizuri alichokionesha katika klabu yake ya Real Madrid na timu yake ya taifa ya Wales.

FIFA pia imetoa orodha ya makocha wanaowania uzo ya kocha bora duniani kwa upande wa soka la wanaume.

Kura za mwisho zitapigwa na makocha na manahodha na makocha wa timu za taifa pamoja na maafisa habari wa mashirikisho ya soka.

Washindi watatangazwa kwenye hafla itakayofanyika Zurich January 11, 2016.

Mapema mwaka huu, Ronaldo alitwaa tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka 2014 kwa mara ya pili akiwapiku Lionel Messi na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer.

Orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2014;

Sergio Aguero (Argentina/Manchester City)
Gareth Bale (Wales/Real Madrid)
Karim Benzema (France/Real Madrid)
Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid)
Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City)
Eden Hazard (Belgium/Chelsea)
Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain)
Andres Iniesta (Spain/FC Barcelona)
Toni Kroos (Germany/Real Madrid)
Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich)
Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona)
Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona)
Thomas Muller (Germany/FC Bayern Munich)
Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich)
Neymar (Brazil/FC Barcelona)
Paul Pogba (France/Juventus)
Ivan Rakitic; (Croatia/FC Barcelona)
Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich)
James Rodriguez (Colombia/Real Madrid)
Alexis Sanchez (Chile/Arsenal)
Luis Suarez (Uruguay/FC Barcelona)
Yaya Toure (Cote d’Ivoire/Manchester City)
Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich)

Orodha ya makocha wanaowania tuzo ya kocha bora duniani;

Massimiliano Allegri (Italy/Juventus)
Carlo Ancelotti (Italy/Real Madrid)
Laurent Blanc (France/Paris Saint-Germain)
Unai Emery (Spain/Sevilla FC)
Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich)
Luis Enrique Martinez (Spain/FC Barcelona)
Jose Mourinho (Portugal/Chelsea)
Jorge Sampaoli (Argentina/Chilean national team)

No comments