Recent Posts

Magazeti Uingereza leo Jumatatu Octoba 19 habari za michezo haya hapa

Newspapers

Dail express limeandika haya

Man united na Totenham wapo kwenye vita kubwa ya kupata huduma ya mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino katika dirisha la usajili mwezi January.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa James Milner ni mchezaji aliyekamilika. Jurgen Klopp:"Ni mchezaji aliyekamilika, wa kimataifa, mashine na kila kitu anacho".

Daily mirror limeandika haya

David Beckham amepanga kucheza mechi saba kwanye mabara saba kwa siku saba kwenye zoezi la uchangishaji fedha na UNICEF.

Radmel Falcao atakuwa tayari kuachana na Chesea mwezi January. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa hana raha klabuni hapo kutokana na kutokupewa nafasi ya kucheza akiwa yupo kwa mkopo akitokea Monaco.

Daily star limeandika haya 

Louis van Gaal amemuonya Ander Herrera kuhusu kuwa nyota kwenye mechi dhidi ya Everton hakutamhakikishia namba ya kudumu man united kama kiungo.

Kipa mpya wa Chelsea Marco Amelia ameonyesha ujasiri mkubwa baada ya kuchukua simu yake na kumpigia kocha wake Jose Mourinho baada ya kusikia kipa chaguo la kwanza Courtois atakuwa nje mpaka Christmas baada ya kupata majeraha.

The Gurdian limeandika haya

Mshambuliaji wa Manchester City Wilfred Bony amekubali kuwa aliugua malaria kipindi cha kiangazi. Bony alishindwa kusafiri na man city pre season tour  Australia na Vietnam kutokana na ugonjwa huo.

SOURCE SKY SPORT

No comments