PIGO KWA BERCELONA HILI HAPA
Mchezaji wa Barcelona Lionel
Messi amepata pigo kubwa kwake mwenyewe na timu yake
baada ya kuumia kiungo cha ndani ya goti na katika mchezo wa timu yake ilipoifunga Las Palmas kwa magoli 2-1 jumamosi hii.
baada ya kuumia kiungo cha ndani ya goti na katika mchezo wa timu yake ilipoifunga Las Palmas kwa magoli 2-1 jumamosi hii.
Messi ambaye aligongana na
mchezaji beki wa Las Palmas, Pedro Bigas katika dakika ya tatu,
aliendelea kucheza lakini akashindwa kuendelea nakuomba kufanyiwa
mabadiliko katika dakika ya nane ya mchezo.
Baada ya kupelekwa hospitali,
imefahamika kuwa atakaa nje ya uwanja kwa takribani week 7-8. Messi
ameumia kiungo katika goti lake kitaalam ‘collateral ligament tear’.
Kocha wa Barcelona, Luis Enrique
amesema hakuna kitu kibaya kama majeruhi kwa mchezaji, lakini akasema
taarifa hizi ni njema kwa wapinzani wao.
Messi alitibiwa maumivu yake mara
ya mwisho 2013 na kurudi katika fomu yake vizuri huku akiweka rekodi ya
kuwa mfungaji bora wa klabu wa muda wote.
No comments