STAND UNITED YAELEZEA HATMA YA KOCHA WAO
Baada ya taarifa kuzagaa kuwa
benchi la ufundi la timu ya Stand United ‘Chama la wana’ limevunjwa
ambalo lipo chini ya mfaransa Patrick Liewig, afisa habari wa timu hiyo
Deokaji Makomba ameiuka na kukanusha vikali taarifa hizo akiita ni
uvumi.
“Mimi nikwambie hakuna taarifa
inayozungumza kuwa benchi la ufundi linavunjwa, benchi la ufundi liko
palepale chini ya kocha Patrick Liewig na akishirikiana na Athumani
Bilal ‘Bilo’, Mathias Lule kasafiri kidogo kaenda kwao Uganda kwa siku
kadhaa lakini baadae atarudi tutakuwa nae” amesema Makom
ba.
ba.
“Benchi letu la ufundi
halijavunjwa, tunaliamini kupoteza mechi mbili ni hali ya mchezo
kwasababu wewe unajipanga hivi mwenzako anajipanga vile anachukua pointi
kwahiyo tuko vizuri tunaendelea kujiandaa ili kuwa bora katika ligi ya
Vodacom”.
No comments