Recent Posts

MAMBO YAPO HIVI JUVENTUS


download (1)
Massimiliano Allegri kocha wa mabingwa watetezi wa Serie A Juventus amekasirishwa na kitendo cha kikosi chake kutoka draw ya goli 1-1 dhidi ya Frosinone na kuendelea kuwapa nafasi Inter Milan kuongoza ligi.
Juve wameonekana kupata shida kwenye mwanzo wa msimu kutokana na kutoka draw mechi mbili na kufungwa mechi mbili wakati wao wapo kwenye mbio za kutetea ubingwa wao.
“Sio tu nimekasilishwa na haya matokeo bali pia inanivunja moyo.
Tunaitaji pasi nyingi na kidogo sana mchezo wa mmoja mmoja. Tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwasababu sasa hivi sisi timu ambayo tunaweza kuifunga timu yoyote lakini pia tunaweza kufungwa na timu yoyote. Tunapoteza point nyingi sana na sifurahii jambo hili” ,alisema kocha huyo akiongea na TV moja huko Italy

No comments