COUTINHO WA LIVERPOOL HATIHATI KUJIUNGA NA BERCELONA
Kiungo nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Filipe Coutinho anapigiwa chapuo la kuihama klabu hiyo na kujiunga na miamba ya soka nchini Hispania klabu ya soka ya Barcelona.
Hali hiyo imek
uja baada ya Neymar wa Barcelona kuulizwa ni mchezaji gani wa taifa lake angependa ajiunge naye mjini Catalunya, Neymar bila kusita alimtaja Coutinho kuwa itakua ni usajili mzuri kwa klabu na pia kwa mchezaji mwenyewe.
Maofisa wa usajili wa Barcelona tayari walikwisha fanya mikutano kadhaa na wenzao wa Juventus kuhusu uwezekano wa kutaka kumsajili kiungo Paul Pogba lakini huwenda usajili wa Coutinho ukawa mwepesi zaidi.
Mchezaji mwingine aliyetoka Liverpool, Luis Suarez naye ni moja ya wachezaji wanaomkubali sana Coutinho na wakati akiondoka Liverpool msimu wa 2014/15 alimuomba nahodha Steven Gerard kumpa uangalizi Coutinho.
Taarifa hizi sio nzuri kwa mashabiki wa Liverpool ambao wamekua wakishuhudia kuondoka mfululizo kwa mastaa wake akianzia Luis Suarez na msimu huu Raheem Sterling.
No comments