TEVEZ AMVUNJA MGUU MCHEZAJI EZEKIEL HAM
Mshambuliaji wa zamani wa Juventus na klabu za Manchester, Carlos Tevez ameomba radhi baada ya kumvunja mguu mchezaji Ezekiel Ham wa Argentinos Juniors timu yake ya Boca Junior ikiibuka
mshindi wa mabao 3-1.
Tevez ambaye hakua na mchezo mzuri siku hiyo aliwania mpira wa 50-50 na Ham na kusababisha kuvunjika mguu kwa mchezaji huyo ambaye hata hivyo hakupewa adhabu yeyote kutokana na tackling hiyo.
Tevez aliwahi haraka sana kuomba msamaha kwa kilichotokea huku akionesha kusikitika kwake kwa kumrudisha nyuma Ham. Lakini kocha wa Argentinos Junior amesema haamini kama kweli Tevez hakukusudia kumuumiza Ham.
Tevez amesema anajutia kwa maana alienda kwa ajili ya mpira huku akijitetea kuwa hajawahi muumiza mtu yeyote katika career yake ya soka.
Tevez mwenye miaka 31 aliamua kurudi nyumbani mara baada ya kuvichezea vilabu vya West Ham, Manchester United na City pamoja na Juventus za barani Ulaya.

No comments