MANARA:YANGA HAWATAZUNGUMZA MILELE BAADA YA MECHI YA JUMAMOSI
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema uongozi wa Yanga hautapata nafasi ya kuzungumza kabisa.
Uongozi wa Yanga umeamua
‘kuvikaushia’ vyombo vya habari kwa madai kwamba wanataka kuzungumza baada ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Simba.
‘kuvikaushia’ vyombo vya habari kwa madai kwamba wanataka kuzungumza baada ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Simba.
“Wanakutana na wafalme wao ndiyo maana wameamua kukaa kimya. Watakaa kimya sana na hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza tena.
“Watakuwa na kipi cha kuzungumza wakati watakuwa wamefungwa. Acha waendelee kukaa kimya,” alisema Manara.
Mashabiki wengi wa Yanga wamekuwa wakilalamika kuona Yanga wakiwa kimya bila ya kuzungumza lolote.
Baadhi wamekuwa wakisema huenda Yanga wanataka kutosema lolotea kwa kuwa wanajua Simba ni wenyeji.
Badala yake, vyombo vya habari wamekuwa wakiwahoji mashabiki wa Yanga ambao wanazungumza kama viongozi.
Source;salehjembe
No comments