Recent Posts

KOCHA WA SIMBA AKATAA MECHI YA KIRAFIKI NA SABABU NDIO HII HAPA

Dylan Kerr kocha mkuu wa Simba SC
Wakati homa ya pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ikiwa inazidi kupamba moto mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa siku ya Jumamosi.
Kiongozi wa klabu hiyo Abdul Mshangama amesema kocha kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr amekataa kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuwavaa Yanga lakini pia akieleza hali ya kambi  huko visiwani Zan
zibar.
“Kocha ameamua tusicheze mechi yoyote ya kirafiki ili kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kufanya mazoezi, utakuta asubuhi tunafanya mazoezi kwa masaa matatu halafu jioni tunaenda kwenye fukwe za Zanzibar kwahiyo hakuamua wachezaji wacheze mchezo wa kirafiki akihofia ‘injuries’”, amesema Mshangama.
“Kambi inaendelea vizuri na wachezaji wote wako katika hali nzuri, Banda jana amefanya mazoezi kwenye ‘session’ zote mbili. Morali iko juu sana na wachezaji wanatamani siku hiyo ifike tucheze na watani wetu wa jadi naamini mchezo utakuwa mzuri sana”.

No comments