Recent Posts

BERCELONA INAWEZA ISISHIRIKI TENA LIGI YA HISPANIA HILI LIKIFANIKIWA

Rais wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA) Javier Tebas na waziri wa michezo wa Hispania Miguel Cardenal wamethibitisha kamaCatalonia ikijitenga na kutoka katika umoja wa Hispania klabu
ya FC Barcelona ambayo inatokea Cataloniahaitashiriki Ligi Kuu Hispania.
Waziri huyo wa michezo amethibitisha kama Catalonia watajitenga na Hispaniabasi klabu ya FC Barcelona haitapata fursa ya kushiriki michuano ya soka yaUlaya. Uchaguzi mkuu wa kikanda waCatalonia unatarajia kufanyika September 27.
Waziri wa michezo wa Hispania Miguel Cardenal
Catalonia wameingia katika mvutano usio rasmi na baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vinashawishi Cataloniakujitenga na umoja wa Hispania. Hilo linaweza kutokea kama miongoni mwa vyama hivyo vitashinda viti vingi katika bunge la Catalan.
Rais wa Ligi Kuu Hispania Javier Tebas

No comments